Mwezi huu wa tatu, tufanye uwe wa mafanikio kwenye biashara zetu. najua kila mtu ana idea zake za kufanya biashara gani na wapi pa kupitia, ila naona baadhi ya watu wengi bado wanawaza idea zile zile za nguo/mitumba na kuwekeza hela zao zote huko (ndio maana nimeweka picha ya nguo hapo juu).

Personally hadi leo sijaingia kwenye biashara ya kuuza nguo naweza nikaamua siku just as a challenge ila kwa sasa na avoid, kwa maana haileti maana kwa mfanyabiashara mdogo anaetaka kupata faida mapema, kwanza competition ni kubwa sana, pili kuna variable nyingi za kuchagua nguo aina gani, wanaume au wanawake, size ipi, rangi ipi itapendwa, style ipi itapendwa, vitu vingi sana vya ku consider.

Mtu anaona kisa kila mtu ana vaa nguo basi nguo ndipo biashara ya kuingia. Lakini kuna factor nyingi sana ambazo zitakufanya usiingize hela mapema, inahitaji ujijenge mda mrefu ili upate loyal customer base kwenye biashara yenye competition kubwa kama nguo, so hauto ingiza hela nzuri atleast mwaka wako wa kwanza au wa pili. anyway these are just thoughts, na nimepewa ushuhuda pia na watu ambao wamejaza tu mitumba na haiendi wala nini.

so kwa wale wanaotaka kupata ideas za bidhaa ambazo personally nadhani zina uwezekano mkubwa kuuza na hata mimi ningekua na mda zaidi ningezifanyia kazi hizi hapa chini tano.

1.Kitchen supplies

Hamna kitu ambacho kinachosha kama kukatakata vitu kwa ajili ya kupika, kuandaa mboga, viungo ni kazi kweli. So mtu nikiwepo mimi mmoja wapo nikiona vitu vinavyoweza rahisisha kazi hii, bila kuwaza mara mbili nanunua. So ukiweza fanya biashara mtandaoni tu bila kuwa na duka, kuna uwezekano mkubwa wa yeye kufanikiwa na kuuza vingi sana ndani ya mda mdogo.
mifano hii hapa.

2.electronic cigarettes (e-cigarettes)

Mimi personally sivuti sigara, na sitegemei kujishughulisha na chochote kinachohusiana na sigara, but hii inaweza kuwa ni opportunity kubwa. hizi sigara za electronic hazitumii tobacco kama sigara za kawaida, na wala sio shisha(sheesha/hookah) maana nazo hutumia tobacco zenye ladha madhara yaleyale kwenye shisha, e cigarates pia hazina tar, hazina majivu, wala harufu mbaya. so e-cigarates husemwa kuwa ni salama kuliko kuvuta sigara kwa kuwa zinatumia nicotine na flavour, na ni nzuri sana kwa watu wanaotaka kuacha kuvuta sigara kwa maana inawapa hisia zilezile za kuvuta sigara bila madhara yote ya sigara. pia ina flavour kama za shisha ila madhara haina kama shisha. Kwa mtu atae taka kufanya hii afanye research zaidi, search google e-cigarates au electronic cigarates. kuna makala nyingi sana za kuzielezea kwa maana nchi nyingi za wenzetu zimeshakua ni kitu cha kawaida, ila huku naona pengo lipo na watu wanaendelea kujiua tu na sigara.

mfano wake ni hizi hapa

3.Usb wall outlets

Hapa ni mambo ya umeme sasa, outlet za usb zinakuja juu sana kila sehemu, watu wanatembea na waya tu sikuhizi. ukiwa una simu yako mfukoni hauhitaji kubeba vichwa vya kuchajia, usb outlet ndio zimebadilisha mchezo mzima wa kuchaji simu, i can see watu wenye ma bar/restaurants/sehemu za chakula/coffee zikihitaji hizi outlet kwa ajili ya wateja wao, nyumbani pia, ofisini pia itasaidia sana.

mfano ni hizi hapa.

 

4.LED lights

Led light ni soko la kipekeake ambalo ndani lina category nyingi sana, sijaona mtu ambae amejaribu ku ingia vizuri kwenye hili soko, so competition ni ndogo sana na bidhaa zipo na siyo mpya kwa maana nchi zingine watu wamesha adapt hizi light za LED kwenye maisha yao ya kila siku.

i) kuna bulb za kawaida ambazo zinatumia umeme mdogo sana kuliko bulk za kawaida (florecent), na zinatumia umeme mdogo sana kuliko hata tube light zile, kuliko hata zile nyeupe zile (CFL) so hapo kwenyewe tu ni selling point kubwa, na kuna nakala kibao ziki prove hili jambo. LED bulb pia hazitoi joto, na ni bei ndogo kuliko zote zingine, na zina kaa mda mrefu kuliko bulb aina zote zingine. cheki picha hii yenye mahesabu kidogo.

5. iphone accesories store

Vifaa vya simu milele vitauza, hapa ni kama nguo tu, uzuri wa vifaa vya simu ambao ni tofauti na nguo ni kwamba kwanza ni vidogo, mtaji unaweza ukaanza nao kwa gharama ndogo uwezavyo, hata elfu 50 ukiwa nayo ni mtaji tosha kuugeuza kuwa laki 2 ukichagua vifaa vya simu vinavyofaa, na wengi wanapo boogie ni kushindwa ku ji clasify vizuri anataka auze vifaa vya simu vyote, sasa hapa ndipo utapoweza teka soko kwenye vifaa vya simu kwa mtaji mdogo, shikilia soko dogo ila ulishikilie vizuri, usiuze phone accesories tupu, bali uza kwa ajili ya iphone, ma cover, screen protectors, earphone original,charger original na mengine mengi.

Kuna watu wengi wananicheki kuniuliza mi nina mtaji mdogo nianzie wapi, hii number tano kuna wengi wataweza idharau ila ukiwa na mtaji wa 50,000 hadi 200,000 unaweza ukaanza na hii as soon as possible na kutengeneza hela nzuri tu. apple ni kampuni inayopendwa, watumiaji wa simu hizi hawatumii simu tu, wanatumia brand wanapenda wapate vitu vizuri kwa ajili ya simu zao, so watumiaji wa iphone ni soko tosha kwa mfanya biashara anaeanza tu.

 

watu wengi wana niuliza for ideas ya wapi pa kuanza, bidhaa gani naona zinaweza kuuza vizuri. hii list ni moja wapo tu nitaendelea kutoa idea za bidhaa zingine as time goes. Kuna njia nyingi za kutafuta bidhaa zenye uwezo wa kuuza na njia hizi naziongelea kwenye course na mengine mengi sana.

I hope hii itawapa idea baadhi ya watu, na wengine wajue kwamba masoko yapo mengi sana ya kuweza kufanya biashara na kuingiza hela nzuri tu ya pembeni huku unafanya kazi zako, ni uwezo wa kujipangilia na kufuatilia vizuri trend na bidhaa.

Nitakua naandika post zingine kuwapa ideas za bidhaa, nilijulishe mawazo yako kuhusu hizi kwenye comments hapo chini.

Facebook Comments

Comments 4

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

 • nkilijiwa

  March 5, 2017 | Reply

  Nashukuru kwa mafunzo yako unayotoa yanatujenga ki fikira postive

 • Fulgence Kandegukila

  March 15, 2017 | Reply

  Ahsante mkuu kwa mawazo yanayonifungua akili yangu .keep it up

 • obeid

  March 20, 2018 | Reply

  mimi nieleze tu namna ya kuagiza mzigo online ili nianze na mtaji wangu wa elfu 50

 • James Dogani

  November 18, 2018 | Reply

  Ee bwana nimependa andiko lako, kama ni marks ninakupa A+ . Hongera sana , Naomba nikutafute.

 • Leave a Comment